UCHAMBUZI WA RIPOTI YA TUME YA JAJI CHANDE KUHUSU MATUKIO YA OKTOBA 2025

Ndugu waandishi wa habari

Asasi za Kiraia na Watetezi wa Haki za Binadamu tunajukumu kubwa katika jamii la kulinda na kuteta haki za binadamu pamoja na kufuatilia maswala ya uwajibikaji na utawala bora. Baada ya Tume iliyoundwa na Rais Samia Suluhu ya kuchunguza matukio yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 kutoa taarifa yake hadharani tarehe 23/4/2026, tumeona tunawajibu wa kuichambua na kutoa taarifa fupi kwa umma juu ya uchambuzi wa awali wa taarifa hii. Taarifa hii inalenga zaidi kuonesha mapungufu yaliyojitokeza katika taarifa hii na pia kutoa mapendekezo nini kifanyike.

Pamoja na kwamba toka awali hatukukubaliana na muundo wa tume hii ambao haukuzingatia ushirikishwaji wa makundi yote ya kijamii na wataalamu wa kimataifa wa uchunguzi wa matukio ya namna hii, bado tunawajibu pia wa kuchambua taarifa hii na kutoa mapungufu yake na kutoa mapendekezo yetu.Read more...https://thrdc.or.tz/online-center/other-publications-views